CRIMEA WAPIGA KURA KUJIUNGA NA URUSI
Wabunge wa Mji ulio kusini mwa Ukraine,Crimea wamepiga kura ili kuwa sehemu ya Urusi.
Bunge limesema uamuzi huo utaachwa mikononi kwa watu wa Crimea kwa ajili ya kupiga kura ya maoni tarehe 16 mwezi Machi.
Serikali ya Kiev imesema inaamini kuwa Crimea kujiunga na Urusi ni kinyume na Katiba.
Crimea, ambayo wakazi wake walio wengi wana
asili ya Urusi, imekua katika malumbano baada ya kuanguka kwa Rais wa
taifa la Ukraine.
Taarifa ya Bunge la Crimea imekuja wakati
viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kujadili hatua ya
kupeleka vikosi vya Urusi katika ardhi ya Ukraine.
No comments:
Post a Comment