LOWASSA, CHENGE WAMSIFU SITTA
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amemsifu Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akisema anazo sifa za
kuliongoza Bunge Maalum la Katiba na kuiwezesha Tanzania kupata katiba
mpya.
Naye Mjumbe wa Bunge hilo, Andrew Chenge, amesema kuwa tofauti zilizokuwapo kati yake na Sitta wakati wa kinyang’anyiro hicho zimekwisha.
Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM) alisema hayo katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya Waziri Sitta kuibuka mshindi katika uchaguzi huo, uliofanyika bungeni juzi.
Lowassa alisema kuchaguliwa kwa Waziri Sitta kuwa mwenyekiti wa kudumu wa Bunge hilo kutawezesha mchakato wa kuijadili Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanikiwa na hatimaye Watanzania kupata katiba iliyo bora.
“Huyu ni mwenyekiti wa viwango na kasi...na ameahidi kwamba, atatekeleza viwango na kasi...matumaini yangu kuwa tutafanikiwa,” alisema Lowassa.
Akizungumzia uchaguzi wa mwenyekiti wa kudumu wa Bunge hilo, Lowassa
alisema ulipangwa vizuri na wagombea wote wawili waliowania nafasi hiyo
walikuwa wazuri, ingawa Waziri Sitta alikuwa bora zaidi.
“Nadhani uchaguzi huu wa mwenyekiti utatupeleka mbele zaidi...na mambo yatakwenda kwa kasi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali,” alisema Lowassa.
“Nadhani uchaguzi huu wa mwenyekiti utatupeleka mbele zaidi...na mambo yatakwenda kwa kasi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali,” alisema Lowassa.
Mjumbe mwingine aliyewania nafasi hiyo pamoja na Waziri Sitta, ni
Hashim Rungwe, ambaye alipata kura 69 sawa na asilimia 12.3 dhidi ya
kura 487 (asilimia 86.5) alizopata waziri huyo. Kura saba, sawa na
asilimia 1.2 ziliharibika.
No comments:
Post a Comment