MZOZO WA KIDIPLOMASIA
KATI YA KENYA NA SOMALIA
Mzozo wa kidiplomasia unanukia kati ya Kenya na
Somalia baada ya polisi kumkamata kimakosa mmoja wa maafisa wakuu wa
ubalozi wa Somalia nchini Kenya Siyad Mohamud Shire .
Tayari balozi wa Somalia nchini Kenya Mohamed
Ali Nur ameitwa na serikali yake kueleza matukio yanayoambatana na
kukamatwa kwa raiya wa asili ya kisomali ambao serikali inasema baadhi
yao hawana vibali vya kuishi nchini.
Maafisa
wa polisi nchini Kenya wamekuwa wakiendelea na msako wao dhidi ya
wahamiaji haramu na wale wanaoshukiwa kushiriki matendo ya kigaidi na
uhalifu.
Hata hivyo serikali ya Somalia imesikitishwa nao
kwa kumkamata afisa wa ubalozi wa Somalia anayeshughulikia masuala ya
kisiasa Siyad Mohamud Shire.
Kwa sababu hiyo Somalia imetuma taarifa katika
vyombo vya habari ikisema kuwa waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed
amefanya mazungumzo na balozi wa Somalia nchini Kenya aliyefika
Mogadishu hapo Jumapili kumweleza hatma ya raiya wa Somalia wanaoishi
Kenya katika msako unaoendelea.
Japokuwa serikali ya Kenya kupitia kwa wizara ya
usalama wa kitaifa imekuwa ikishikilia kuwa hailengi jamii yoyote
katika kuwakamata raiya wa kigeni na kuwarejesha katika nchi zao ama
kambi za wakimbizi.Taarifa hiyo imeanusha hilo na kusema maafisa wa polisi wamekuwa wakiwazuilia wasomali wengi na kuwatesa.
Tukio la kumnasa, Bwana Siyad Mohamud Shire limechukuliwa na serikali ya Somali kuwa ukiukaji mkubwa wa mkataba wa kidiplomasia.Inasemekana kuwa bwana Shire alikamatwa na kuzuiliwa na polisi kwa muda licha ya kuwa na kitambulisho cha kazi.
Mkutano kati ya waziri mkuu wa wa Somali na
balozi wa Kenya ulifanyika baada ya baraza la mawaziri kuandaa kikao
kisichokuwa cha kawaida kujadili hali ilivyo Kenya.
Juhudi za kumpata waziri wa mambo ya nje wa
Kenya balozi Amina Mohamed kueleza msimamo wa serikali hazikufaulu ila
maafisa wa polisi walikataa kuzungumzia suala hilo wakisema kuwa
litashughulikiwa na ngazi ya juu.
Polisi nchini Kenya walianza msako kote nchini
wiki tatu zilizopita baada ya matukio mengi yanayoambatanishwa na ugaidi
ama uhalifu kutokea huku zaidi ya watu kumi wakifariki baada ya
milipuko kadhaa kutokea katika mtaa wa Eastleigh na maeneo jirani jijini
Nairobi.
Kisichojulikana kwa sasa ni namna nchi zote mbili zitakavyoendelea kushirikiana kidiplomasia katika mazingira yaliyopo.
EVERYBODY READ THIS TESTIMONY ON HOW I GOT MY LOAN FROM A LEGIT AND TRUSTED LOAN COMPANY My name is Kjerstin Lis, I have been searching for a loan to settle my debts, everyone I met scammed and took my money until I finally met Mr, Benjamin Breil Lee He was able to give me a loan of R 450,000.00.He also helped some other colleagues of mine. i am talking as the happiest person in the whole wide world today and i told my self that any lender that rescue my family from our poor situation, i will tell the name to the whole wide world and i am so happy to say that my family is back for good because i was in need a loan to start my life all over as i am a single mum with 3 kids and the whole world seemed like it was hanging on me until i meant the GOD sent loan lender that changed my life and that of my family, a GOD fearing lender, Mr, Benjamin, he was the Savior GOD sent to rescue my family and at first i thought it was not going to be possible until i received my loan, i invited him over to my family get-together party which he did not decline and i will advise any one who is in genuine need of a loan to contact Mr, Benjamin Breil Lee via email at (247officedept@gmail.com ) because he is the most understanding and kind hearten lender I have ever met with a caring heart. He doesn't know that i am doing this by spreading his goodwill towards me but I feel I should share this with you all contact the right loan company Email via: 247officedept@gmail.com or whatsapp +1-989-394-3740. .
ReplyDelete