683 WAHUKUMIWA KIFO MISRI
Jaji wa mahakama nchini Misri, amewahukumu kifo watu 683 akiwemo kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie.
Mawakili wa watuhumiwa wanasema kuwa wateja wao
walikabiliwa na makosa mengi yakiwemo, kushambulia kituo cha polisi
mjini Minya mwaka 2013 ambapo polisi mmoja aliuawa.
Jaji huyo pia alibatilisha hukumu ya
kifo iliyotolewa kwa watu 492 kati ya watu 529. Hukumu hiyo ilipitishwa
mwezi Machi na sasa watahudumia kifungo cha maisha jela.
Kesi na kasi ya kuzisikilizwa kwa kasi hizo,
imesababisha hasira na kukosolewa na shirika la kutetea haki za binadamu
la Umoja wa Matifa UN.
Kadhalika shirika la Huma Rights Watch
limelalamika kuwa kesi hizo zilisikilizwa tu kwa saa chache huku
mahakama ikiwazuia mawakili kuwawakilisha washitakiwa.
Duru zinasema kuwa jamaa wa watuhumiwa waliokuwa wanasubiri nje ya mahakama walizirai baada ya kupokea taarifa za hukumu hiyo.
Mwezi jana shirika la kutetea haki za binadamu
la Umoja wa Mataifa, lililaani kesi hizo likisema kuwa zinakiuka sheria
ya kimataifa ya haki za binadamu.
Msemaji wa shirika hilo, Navi Pillay, alisema kuwa kesi hiyo ilikumbwa na makosa mengi ya utarataibu.
Maafisa wa utawala nchini Misri wamekuwa
wakiwasaka na kuwakamata wapiganaji wa kiisilamu na wanachama wa
vuguvugu la Muslim Brotherhood ambao walimuingiza mamlakani aliyekuwa
Rais Mohammed Morsi ambaye baadaye aliondolewa na Julai.
Mamia wameuawa huku maelfu ya raia wakikamatwa.
No comments:
Post a Comment