GERMAIN KATANGA JELA MIAKA 12
Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC imemhukumu
kiongozi wa zamani wa wanamgambo waasi katika Jamuhuri ya kidemokrasi
ya Kongo, Germain Katanga, kifungo cha miaka kumi na miwili jela baada
ya kumpata na hatia ya uhalifu wa kivita.
Bwana Katanga alipatikana na hatia ya kuhusika
katika mauaji ya mamia ya wanavijiji katikaeneo la Ituri Katanga mwezi
Machi mwaka 2003.
Jimbo la Katanga ni jimbo lenye utajiri wa
madini ya dhahabu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo . Lakini kiongozi
huyo wa waasi mwenye umri wa miaka thelathini na sita hakupatikana na
hatia ya kuwatumikisha watoto vitani na makosa mengine ya ubakaji.
No comments:
Post a Comment