Friday, 23 May 2014

  UN YASEMA VATCAN INAPUUZA HAKI ZA WATOTO


 PAPA FRANCIS

Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi mateso imelaumu vikali kanisa Catholiki kwa kutoshughulikia ipasavyo suala la unyanyasaji wa watoto ndani ya kanisa hilo.
Katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni na Umoja huo mjini Geneva , Kamati hiyo imeushutumu utawala wa Vatcan kwa kuwahamisha watawa kutoka parokia moja hadi nyingine kuwaepusha kushtakiwa, na kupuuza haki za waathiriwa za kupokea fidia .
Utawala wa Vatican uliithinisha mkataba dhidi ya unyanyasaji , ukatili na matendo yaliyo kinyume na utu.Uchunguzi uliofanywa na kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Vatcan ni sehemu ya uchunguzi wa mara kwa mara wa kamati hiyo dhidi ya nchi wanachama ili kuhakikisha mikataba inatekelezwa.

Kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa ina hofu kuwa wakati utawala wa Vatcan umeelezea kutokubali kamwe kuwepo kwa unyanyasaji ndani ya kanisa, maneno hayaendani na vitendo .

Kamati hiyo imekasirishwa zaidi na kwamba Utawala wa Vatcan unasisitiza kuwa unahusika zaidi na wahudumu wanaofanyika kazi ndani ya Vatcan kwenyewe , kuliko makasisi wake wanaofanyika kazi kwingineko duniani.

Mwezi Januari mwaka huu utawala wa Vatcan ulichunguzwa upya na kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto, baada ya kupokea ukosoaji kama huo kwamba ulishindwa kuwalinda watoto waliokuwa chini ya uangalizi wake.

1 comment:

  1. K8 (bk8) Games - Vntopbet
    K8. K8 (bk8) Games - Vntopbet.com - The world's best online m88 slot game developer, bk8 delivering unique ラッキーニッキー casino games to the people of

    ReplyDelete