Monday, 23 June 2014

TAASISI YA AFYA YASHAMBULIWA NIGERIA


Mlipuko umeripotiwa kutokea katika taasisi moja ya umma ya mafunzo ya afya katika mji wa Kano ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Nigeria.

Duru zinasema kuwa idadi ya watu waliojeruhiwa katika shambulizi hilo dhidi ya kituo cha mafunzo ya afya , bado haijulikani.
Mji huo umewahi kulengwa na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram, ambao wanataka kubuniwe taifa la kiisilamu Kaskazini mwa Nigeria.

Majimbo matatu Kaskazini mwa Nigeria bado yapo chini ya sheria ya hali ya hatari kufuatia miaka mingi ya harakati za wapiganaji hao wa kiisilamu.


No comments:

Post a Comment